John 19:25-27

25 aWakati huo huo karibu na msalaba wa Isa walikuwa wamesimama mama yake, na dada wa mamaye, na Maria mke wa Klopa, na Maria Magdalene. 26 bIsa alipomwona mama yake mahali pale pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, huyo hapo ndiye mwanao,” 27 cKisha akamwambia yule mwanafunzi, “Nawe huyo hapo ndiye mama yako.” Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Isa nyumbani kwake.

Kifo Cha Isa

(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Luka 23:44-49)

Copyright information for SwhKC